Dkt Awatif Abd Al- Rahman 

Dkt Awatif Abd Al- Rahman 

Dkt. Awatif Abd Al -Rahman alizaliwa mnamo mwaka 1939, katika kijiji cha Al-Zarabi, katika jimbo la Abu Tig ya mkoa wa Assiut. Baba yake alikuwa meya wa kijiji hicho na tangu utotoni, amekuwa hodari na kuthaminiwa ambapo Awatif alifika nafasi ya kwanza katika kiwango cha Jamhuri katika elimu ya kimsingi, kisha akaelekea elimu ya maandalizi katika mkoa wa Assiut ambapo alipata nafasi ya kwanza katika kiwango cha Jamhuri, halafu akaelekea elimu ya sekondari huko Kairo; kwa sababu haikupatikana vijijini wakati huo, ambapo alipata nafasi ya kwanza katika kiwango cha Kairo.

 Alisoma katika  Sehemu ya Uandishi wa Habari kwenye Kitivo cha Sanaa katika Chuo Kikuu cha Kairo na alihitimu kwa ufanisi mwakani 1960. wakati ule , Mwalimu wake Khalil Sabbat alimteua  ili kufanya kazi kama mwandishi wa habari katika kitengo cha kisiasa  katika gazeti la Al-Ahram na jarida la Siasa za Kimataifa mnamo kipindi cha kuanzia 1960 hadi 1964, kisha akafanya kazi kama mhariri katika gazeti la Al-Ahram  la kiuchumi mnamo kipindi kuanzia 1968 hadi 1970.

Awatif alifanya vizuri katika kazi ya uandishi wa habari na alifanya mahojiano zaidi ya mia moja na hamsini na mabalozi wengi. pia , alipata shahada ya Uzamili katika maudhui ya uandishi wa habari wa mapinduzi ya Algeria mwakani 1968 AD, kisha akapata Uzamivu katika vyombo vya habari mwakani 1975 AD.

Dkt. Awatif alijiunga katika kitengo cha kitaaluma ndani ya Kitivo cha vyombo vya habari  katika Chuo Kikuu cha Kairo, ambako alikuwa na cheo cha mwalimu msaidizi, kisha profesa katika  sehemu ya Uandishi wa Habari mwakani 1975 AD, kisha profesa msaidizi mwakani 1980 AD.

Kuanzia  miaka 1985 hadi 1987, aliongoza  sehemu ya Uandishi wa Habari katika Chuo cha vyombo vya habari  , kisha alikuwa Makamu Mkuu wa Chuo cha vyombo vya habari kwa Mafunzo ya Uzamili na Utafiti mnamo mwaka 1987.

Alitembelea nchi nyingi za Kiafrika, kama vile Zimbabwe na Afrika Kusini ambapo aliipotembelea mara kadhaa na alipenda sana kutembea sokoni kwa hivi alitembelea zaidi ya masoko  ya kiafrika  37 ndani ya Bara . Dkt. Awatif Abd Al Rahman anasema kwamba: Bara la Afrika lina ustaarabu mwingi unaoendelea, ambao  inapaswa kuijua  badala ya kuzingatia Ulaya tu, nami ninalichukulia kuwa bara la siku zijazo,  linalohitaji umakini wa vizazi vyote vipya, vyuo vipya. , vyuo vikuu na vituo vya utafiti ili kuiweka Afrika kileleni mwa ajenda. .

Ametunga na kuandika vitabu , tafiti na makala kadhaa  zilizochapishwa katika vituo na majarida husika ambazo miongoni mwao ni :-

•kugundua Afrika, (pamoja na wengine), 1961.

•Israel na Afrika 1948-1984 (pamoja na wengine), 1974.

•uandishi wa habari katika Algeria, chuo cha mafunzo ya kiarabu , Kairo, 1978.

•Barua  pepe ya Wasomaji katika uandishi wa Habari ya Kiarabu, (pamoja na wengine), Kituo cha Utafiti wa Kijamii na Jinai, Kairo, 1979.

•Vyombo vya habari Barani  Afrika.

•Jukumu la vyombo vya habari vya Afrika.

Misri na Palestina,  vitabu vya Ulimwengu wa Maarifa, Kuwait, Februari 1980.

•Masuala ya Utegemezi wa Vyombo vya Habari na kiutamaduni katika Ulimwengu wa Tatu, vitabu vya  Ulimwengu wa Maarifa, Juni 1984.

•Utangulizi wa uandishi wa habari wa kiafrika.

uandishi wa habari wa Kizayuni nchini Misri (1897-1954).

•Afrika na maoni ya umma.

•Tafiti za uandishi wa  habari wa  Misri wa kisasa.

•Shule ya Ujamaa ya Uandishi wa Habari: Enzi ya Leninist (1896-1923).

• Tafiti za Mawasiliano na Uandishi wa Habari.

•Wasiwasi wa uandishi wa habari na waandishi wa habari nchini Misri.

•Alfajiri ya uandishi wa habari wa Kiarabu.

• Wanawake waarabu na vyombo vya habari.

•Mradi wa Wazayuni.. Kupenyza kwa Wazayuni ndani ya Misri kutoka 1917 hadi 2017.

• Uandishi wa Habari na Vyombo vya Habari vya Afrika, ambacho kilipata Tuzo ya kitabu Bora zaidi katika Bara la Afrika kwenye Maonesho  ya Kimataifa ya Vitabu ya Kairo ya 51 .

Amepokea tuzo na nishani kadha, zikiwemo:

• Tuzo la Ukombozi wa Kitaifa la Mandela, Afrika Kusini, 1995.

•Tuzo la Sultan Al Owais katika Sayansi ya Jamii na siku zijazo mwakani 1996, kwa kulingana na uteuzi wa Chuo Kikuu cha Kairo.

• Tuzo la Shukrani kwa  Kitivo cha Mawasiliano ya Misa - Chuo Kikuu cha Kairo - Machi 1997.

Tuzo ya kwanza kutoka kwa Kituo cha Tafiti cha Wanawake na Watoto - Bahrain 1998.

• Tuzo la nchi  kwa Ubora wa Kisayansi katika Jamhuri ya Kiarabu ya Misri mnamo 1999.

•Tuzo la chuo kikuu cha Kiarabu kwa kazi zake zote kwa mwanamake mwarabu 2008.

• Tuzo la Shukrani, Chuo Kikuu cha Kairo 2012.

Tuzo la shukurani la nchi kwa  maswala ya Jamii 2014.

Tuzo la Ubora katika maswala ya Jamii, Chuo Kikuu cha Kairo 2017.